Jumatano, 6 Mei 2020

HISTORIA YA SANAMU LA MLINZI (POSTA)



Historia ya Mnara ule ilianza mwaka 1889, kisha, kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 - 1945).
Kwa ufupi Sanamu ya mwanzo kukaa pale ni sanamu ya Herman Von Wissman, Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir Ibn Salim Al Harthi, mtawala/sultani
wa Pangani Tanga.
Baada ya kumteka na kumyonga Abushir, Von Wissman alirejea Ujerumani na kisha baadaye kuteuliwa kuwa Gavana wa Nchi zilizokuwa chini ya Ujerumani za Afrika Mashariki (German East Africa). Alitwaa Dar es Salaam na Pwani nzima, japo alikaa muda mchache Dar es Salaam.
Gavana huyu alifanya utafiti wa kutafuta ni wapi kitovu cha mji wa mji wa Dar es Salaam. Yaani katikati mwa mji kwa vipimo, ndipo alipogundua eneo lile pale Posta na kisha akaagiza pajengwe bustani na Sanamu lake likasimikwa. Inadaiwa pale ndipo palikuwa katikati mwa Dar es Salaam miaka ile.
Inaaminika ndiye aliyetoa wazo la kutengeneza ramani ya kujenga makambi ya wapiganaji ama wanajeshi wa Jeshi la Ujerumani eneo ambalo lilikuwa likiitwa Carrier Corps (Waswahili wakaita Keriakoo/Kariakoo). Ndio maana utaona mitaa ya Kariakoo imenyooka na kujengeka vizuri. Ilikuwa makambi ya wanajeshi.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia iliyopiganwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918 ambapo Waingereza walishinda na kuchukuwa koloni la Tanganyika, mwaka 1916 ndipo Sanamu la Bwana Herman Von Wissman liliondolewa na likawekwa Sanamu la sura ya Askari Mweusi mwaka 1927 kama ishara ya kuthamini mchango wa Askari Waafrika waliopigana kwenye Vita hivyo. Lile Sanamu limedumu hadi leo hapo panapoitwa Askari Monument.
Hiyo ni historia fupi. Yule Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki ilibidi arejee kidogo kwenye historia hii fupi kabla ya kupendekeza kuondoa kwa Sanamu ile na kuweka sanamu ya Diamond. Sanamu ile ina uzito katika Historia ya nchi hii na bado inahitajika kuenziwa na kuhifadhiwa kwa Historia ya Vizazi vijavyo

MY FACEBOOK LINK  BOFYA HAPA

Jumatatu, 27 Mei 2019

MAELEZO KUHUSU FOMU ZA MKOPO

TANGAZO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA NA DIPLOMA MNATANGAZIWA KUWA 
UDAHILI WA FOMU ZA MKOPO UTAANZA HIVI KARIBUNI HIVYO WAHUSIKA WOTE WA FOMU HIZO ZA MKOPO MNATAKIWA KUHAKIKI VYETI VYA KUZALIWA NA VILE VYA VIFO ENDAPO MZAZI AU WAZAZI WAMEFARIKI  HIVYO BASI BAADA YA UHAKIKI MTATUMIWA VYETI VIKIWA NA MUHURI WA RITA    AMBAYO NI MOJA SIFA YA MTU ABAYETAKIWA KUJAZA FOMU YA MKOPO NI LAZIMA ATUME FOMU IKIWA NA CHETI CHA KUZALIWA KIKIWA NA MUHURI WA RITA  KWA MSAADA PIGA SIMU NAMBA 0659873288

Jumamosi, 19 Januari 2019

PATA MUVI MPYA KWA BEI POA

WATANZANIA WOTE PAMOJA NA NCHI JIRANI MNATANGAZIWA  KUWA  WASILIANA NA MWENYE BLOG ILI UPATE MUVI MPYA NA ZA KUSISIMUA AINA ZOTE KWA GHARAMA NAFUU KABISA 0753273288

Jumatano, 2 Januari 2019

TANGAZOTANGAZO TANGAZO


TANGAZOTANGAZO TANGAZO
MNAKARIBISHWA  KWA TUITION YA MASOMO YA COMPUTER, HUDUMA ZA STATIONERY INTERNET CAFÉ, BINDING, LAMINATION, PRINTING, PHOTOCOPY,  UFUNDI WA COMPUTER NA SOFTWARE, SCANING, PHOTOCOPY TYPING ONLINE APPLICATION NA HUDUMA ZA PASPORT SI
INTRODUCTION TO COMPUTER     150,000/=
MS WORD,MS EXCELL, MS PUBLISHERS, MS POWER POINT, MS ACCESS MS WINDOW INTERNET & E-MAILS 
MUDA WA MASOMO
UTACHAGUA KIPINDI KIMOJA TU KATI YA VIPINDI VITATU ASUBUHI , MCHANA AU JIONI
VIPINDI
ASUBUHI
MCHANA
JIONI
KUANZA
07:00-0 AM
12:00 AM
04:00 PM
KUMALIZA
09:00 AM
02:00 PM
06:00 PM
MASAA MAWILI KWA SIKU MOJA KWA KIPINDI KIMOJA JUMATATU MPAKA IJUMAA NA JUMAMOSI NI SIKU YA MAZOEZI AU MITIHANI YA WIKI JUMA PILI NI MAPUMZIKO
MWANAFUNZI ATAPATA HUDUMA YA INTERNET BURE eg kuchat,kusoma e-mail kutumia mtandao mpaka mwisho wa masomo yake na kutunukiwa cheti maalumu.
SIFA ZA MWANAFUNZI
Awe na akili timamu,Awe mtanzania ,Awe amemaliza kidato cha nne –alama  “D” Mbili na kuendelea
MALIPO  (ADMISSION FEE
KIINGILIO                                         5000/=
REGSTRATION FORM                     3000/=
                             ADA                                                 150,000/=                 
JUMLA YA MALIPO YA AWALI NI  158,000/=
MAALI CHUO KILIPO
STENDI KUU YA MABASI RUJEWA BARABARA YA KUINGILIA MAGARI
KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA :0653273288 AU 0753273288


Jumatatu, 15 Mei 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

 Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/05/2017